Tumgik
#madhila
sariaisrael · 1 year
Text
Madhila ya Chelsea, Spurs yafute ukocha wa muda
LIGI Kuu ya England (EPL) inaendelea, ukiwa umebaki muda mfupi kufikia tamati, huku baadhi ya timu kufanya zisivyotarajiwa. Hali hiyo imesababisha wamiliki au viongozi wa klabu kuwafukuza makocha na kupachika makocha wa muda, wakiamini kwamba wangeziiondosha vikosi vya timu husika kwenye unyonge nje ya uwanjani na kuwaoa ufanisi uwanjani. Kama ambavyo madereva wa F1 wanavyoonesha uthamini,…
Tumblr media
View On WordPress
0 notes
magaratimes · 2 years
Text
#ParsToday. | Mzozo wapelekea watu milioni moja kukimbia makazi yao Cabo Delgado Msumbiji
#ParsToday. | Mzozo wapelekea watu milioni moja kukimbia makazi yao Cabo Delgado Msumbiji
Wiki hii wakazi wa Jimbo la Cabo Delgado lililoko kaskazini mwa Msumbiji wanatimiza miaka mitano tangu vurugu kuibuka katika eneo hilo na kusababisha zaidi ya watu milioni moja kuyakimbia makazi yao. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR huko Geneva Uswisi, wakazi wa jimbo hilo wameshuhudia madhila makubwa yakitendeka mbele ya macho yao…
Tumblr media
View On WordPress
0 notes
mwanagenzi · 5 years
Text
Chungu na Pegiko
Kutegemea pegiko, ndio tabia ya chungu Kisipate hangaiko, kikaja tenguka tengu Kama mwana na mbeleko, huwezi engua engu Mambo huenda mtengu, chungu pasi na pegiko ~Utunzi wa Hamisi Kissamvu #Mwanagenzi
Kutegemea pegiko, ndio tabia ya chungu Kisipate hangaiko, kikaja tenguka tengu Kama mwana na mbeleko, huwezi engua engu Mambo huenda mtengu, chungu pasi na pegiko
Chungu pasi na pegiko, itakufika mizungu Utapata hangaiko, huwezi kuvuga dengu Adha yake mnenguko, kila muda nengunengu Mambo huenda mtengu, chungu pasi na pegiko
Chungu pasi na pegiko, ni duni usoni mwangu Inanipa hamaniko, mnani watu…
View On WordPress
0 notes
mazallaposts · 6 years
Link
WADAU wa mradi wa kuwawezesha mabinti na wanawake vijana katika sekta ya elimu wamekutana katikati ya wiki kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UNWomen pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA). Mradi huo ambao umelenga kuondoa vikwazo vya elimu kwa wasichana na wanawake kwa kuangalia sera sheria na kanuni zinazowezesha maendeleo kwa wanawake kwa kuzingatia matakwa ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania imetia saini ulianza mwaka 2016. Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa kusimamiwa na Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya Watu ( UNFPA) unatarajia kuiwezesha Tanzania kuwezesha elimu kwa kutumia mbinu mtambuka kwa kutambua watu wa pembezoni. Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu ofisi ya Unesco Dar es Salaam Faith Shayo akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam Mathias Herman. Mradi huo unatarajiwa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kuwa na uwezo wa kuingia katika utuuzima bila kuvurugwa utaratibu wa upatikanaji wa elimu. Mradi huo unatekelezwa katika wilaya nne za Ngorongoro Sengerema Kasulu na Mkoani huko Pemba. Mkutano huo wa kamati ya ufundi ya mradi ulilenga kutoa ratiba ya utekelezaji wa mradi baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa za utafiti uliofanyika na hali halisi iliyopo nchini kuhusu wasichana na wanawake kwa kuangalia sharia zilizopo utamaduni na tabia. Akizungumza katika mkutano huo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu Dk. Felix Mulengeki alisema kwamba mradi huo utafanikiwa kutokana na ukweli kuwa sharia na katiba za nchi zipo vizuri huku sera nazo zikitambua haki ya kusoma. Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam Mathias Herman akiwasilisha taarifa ya mwaka 2017 ya mradi huo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Wakati mradi unabuniwa ilionekana kwamba kutoeleweka kwa katiba na sheria zilizopo zinazomlinda mtoto wa kike uelewa hafifu umekuwa ukikwamisha maendeleo kielimu kwa watoto wa kike. Dk. Mulengeki alisema kwamba hali ya sera na sheria nchini Tanzania ni salama zaidi kilichobaki utekelezaji wa mradi huo umelenga kukusanya pia takwimu kwa ajili ya kutumika kutengeneza sera. Katika mradi huo unatarajiwa kuongeza uelewa zaidi wa elimu ya afya ya uzazi na kutengeneza mifumo ya kuelimisha watu. Mada mbalimbali zilizojadiliwa ziliwezeshwa kupata muda wa utekelezaji wa vipengele mbalimbali ambavyo vilipaswa kufanyika ili kuondokana na tabia mbaya ambazo zinamnyima binti wa Kitanzania kukamilisha elimu yake. Washiriki wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu wakifuatilia ripoti ya mwaka 2017 ya mradi huo iliyokuwa ikiwasilisha Mathias Herman kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Naye Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) ofisi za Dar es Salaam Faith Shayo amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo na kwamba kamati ya ufundi ya mradi huo ilikutana mara ya kwanza Mei mwaka jana. Naye Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam Mathias Herman anasema kwamba kuna matokeo chanya ya mradi huo. Anasema kwamba madhila mengi ya mabinti katika wilaya hizo zinazofanyiwa utekelezaji wa mradi yamepungua na hali zao kuwa bora kutokana na taasisi mbalimbali zinazohusika na elimu na usalama wa watoto wakike kushirikiana kukabili matatizo waliyonayo. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu Dk. Felix Mulengeki akiwasilisha mada kuhusu sheria na taratibu zinazogusa elimu ya watoto wa kike wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Pia amesema katika suala la elimu ya afya ya uzazi na Ukimwi kumekuwa na mabadiliko kwani taarifa zinakwenda kwa wakati na zinafanyiwa kazi inavyotakiwa na sekta mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali katika kumsaidia mtoto wa kike Aidha amesema kwamba vitini vya kufundishia elimu mbalimbali ambazo zimo katika mradi zimeshafanyiwa kazi na kusambazwa. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Socologia na Anthropologia Dk. Nandera Mhando akiwasilisha uchambuzi wa mradi wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO Ofisi za Tanzania Christophe Legay (wa kwanza kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Mwakilishi kutoka UN Women Bi. Usu Mallya akifafanua jambo katika majadiliano wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Mratibu wa Elimu Shule za Msingi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Salvatory Alute (katikati) akishiriki majadiliano wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay akitoa maoni wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Adam Chacha kutoka kitengo cha Elimu ofisi za Unesco Dar es Salaam akiuliza swali wakati wa mawasilisho ya mada mbalimbali katika mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni washiriki wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption]
0 notes
sariaisrael · 4 years
Text
Corona na madhila ya kujifungia ndani Uingereza
MAISHA yamebadilika sana; watu hapa Uingereza sasa tunaishi katika hali iliyo ngumu kuzoeleka kutokana na mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha maradhi ya homa kali ya mapafu, maarufu kama COVID-19.
Si baba, mama, bibi, babu wala watoto wadogo wanaojiona salama na tangu Waziri Mkuu Boris Johnson atoe tangazo la kuiweka Uingereza yote katika kujifungia ndani au lockdown kama wenyewe wanavyoita, basi maisha yamegeuka magumu na kiza kinene kimetanda.
Watu wamo ndani tu; hakuna kwenda kazini isipokuwa zile muhimu ambazo lazima ziendelee kama madaktari, manesi na wauguzi wengine au wauzaji wa mahitaji muhimu. Wengine sote tumeambiwa tukae ndani na kutulia, kujikinga kwa kunawa kila mara na ikibidi kuvaa barakoa kujikinga na kukinga wengine.
Hakuna kutembeleana; mitaa imekuwa tupu sana na vitakasa mikono vimekuwa ndio mpango mzima hapa. Maduka yanayouza bidhaa ambazo zinaelezwa kwamba si za lazima sana kama kwa sasa, kama nguo, vifaa vya kielektronki pamoja na huduma za maktaba, viwanja vya michezo na gyms za nje zimelazimika kufungwa.
Wataalamu na viongozi wanaendelea kufuatilia hali hii mbaya ya ugonjwa unaoendelea kuambukiza watu na kuua wengine hapa na kwingineko ili kuona kama tarehe iliyowekwa ya marufuku ya mikusanyiko hadi mwishoni mwa mwezi huu itaweza kuondolewa au kuongezwa kulingana na hali ya maambukizi na udhibiti wake.
Watu wanatakiwa kutoka kwa uchache kabisa kama ni kwenda kununua chakula, dawa na vitu vingine walivyopangiwa na hayo yanatakiwa kufanywa kwa uchache kabisa. Waziri Mkuu alilihutubia taifa muda mfupi kabla ya yeye mwenyewe kuambukizwa virusi hivyo kwamba ilikuwa wazi watu zaidi wangeendelea kufariki dunia kwa janga hili.
Watu walio na dalili za COVID-19 wanatakiwa wenyewe kuchukua hatua za kujitenga kabisa (self-isolate) na wengine kupata tiba za magonjwa nyemelezi, kwa sababu ugonjwa huo wenyewe hauna tiba wa kinga. Wanatakiwa kuvaa barakoa ili kuzuia kuambukiza wengine.
Self-isolation ndiyo njia mwafaka na rahisi kukinga wengine kuambukizwa virusi hivyo vilivyoanzia Wuhan nchini China na kusambaa katika nchi nyingi duniani, vikiua zaidi nchini Italia.
Maagizo ya Shirika la Huduma za Afya kwa Umma (PHE) ni kwamba lazima watu wabaki majumbani mwao, hakuna kwenda kazini, shuleni wala kwenye sehemu za mikusanyiko ya umma. Hakuna kutumia usafiri wa umma bila sababu maalumu kama matabibu. Kwa maana hiyo tunachoshuhudia hapa ni utupu katika utoaji huduma kama za mabasi, treni na tyubu na hata teksi.
Ili mmoja atoke lazima awasiliane na watu wa PHE ambao ni wataalamu watakaopima umuhimu wa kutoka na iwapo ni salama. Kama mimi sasa ni zaidi ya wiki tangu nimeacha kwenda kazini na huko wamekuwa kila mara wakipulizia dawa (fumigate).
Ujumbe ulifikishwa kwa wamiliki wote wa simu juu ya amri ya katazo la kutoka majumbani kwa ajili ya afya, usalama wa mwenye simu na watu wengine. Wenye dalili hapa wanaambiwa kwamba wajitenge kwa siku saba ili kuona kama virusi hao wapo na wataanza kuleta matata mwilini.
Kwa anayetokea akawa anaishi na mtu mwenye virusi vya corona hapa, sharti ni kujitenga kwa siku 14 ambazo ndizo huchukua kwa wingi kuweza kuonesha dalili za mwathirika. Serikali sasa inachukua hatua zaidi, ikiwa ni pamoja na kuandika barua na kuzituma katika majumba ya wakaazi kueleza ni akina nano watakaotakiwa kujitenga kwa walau wiki 12 – ikisema ni ‘kujiondoa kwenye jamii’.
Yeyeote aliye kwenye jamii hiyo atapewa angalizo kali sana juu ya kukaa ndani na kuepuka kuwasiliana uso kwa uso na mtu. Hawa wanazuiwa pia kutoka nje kwa ajili ya kufanya manunuzi ya chakula, dawa au mambo mengine ili kuhakikisha kukutana ni sawa na sifuri.
Hawa wa jamii hii ni pamoja na watu wenye magonjwa makubwa ambayo yatawaweka katika hatari kubwa ya kupigwa na virusi hivyo na uwezekano mkubwa ni kupoteza maisha. Wazee wanaofikia kuanzia umri wa miaka 75 na watu wenye magonjwa kama kisukari na mengineyo.
Watu wanaandikiwa barua za kujitenga kwa hadi wiki 12, ukiachilia mbali hao wazee ni wale wenye ugonjwa wa saratani ya mapafu ambamo virusi hawa huenda kushambulia, watu waliopandikizwa viungo vilivyoshindwa kufanya kazi sawa sawa kama mapafu, ini, moyo, figo na kongosho.
Hayo ndiyo maisha ya hapa kwa sasa, na kwa hakika inatisha na sintofahamu iliyopo bado ni kubwa. Kila mmoja anasali kuomba hali hii imalizike na maisha yarejee kama kawaida. Watu wenye saratani wanaoendelea kuchomwa mionzi – kemotherapi au radiotherapy kwa ajili ya saratani ya mapafu wanahusika.
Lakini pia watu wenye saratani ya damu au ya kwenye uteute unaokaa kwenye maungio ya mifupa wakiwa katika hatua yoyote ya matibabu wanatakiwa kutulizana nyumbani kwa wiki hizo 12 na matabibu watawafikishia dawa huko huko.
Wengine ni wale wenye saratani ya kwenye protini zao na wengine ambao kwa ujumla hali yao imepunguza nguvu ya kinga ya miili yao. Kadhalika katika kundi hili ni wenye matatizo ya mfumo wa hewa na kupumua, wenye pumu, wajawazito wenye matatizo ya moyo kwa sababu kimsingi hawa watashambuliwa na kuumizwa zaidi na virusi hawa kama si kupoteza maisha kabisa.
Inavyoendelea sasa, ikiwa ni pamoja na kwa baadhi ya watu ninaowafahamu, ni kwamba wanavyojitenga ikiwa wanaishi kwenye familia moja au kundi, ni mhusika kujitenga chumbani kabisa na akienda kujisaidia awe amevaa barakoa.
PHE wanashauri kwamba wagonjwa au wanaohisiwa kuwa na virusi hawa wakae kwenye chumba chenye hewa ya kutosha – yaani kuwe na madirisha au uwazi ili kwamba hewa iingie na kutoka lakini ihakikishwe kwamba wanatenganishwa na wengine walio wazima na pia matumizi ya bafu na maliwato yawe tofauti.
Ikiwa ni nyumba isiyokuwa na bafu la ziada kwa ajili ya mgonjwa imeshashauriwa kwamba uwekwe mpango wa rota kwa ajili ya kunawa au kuoga ambapo mgonjwa awe wa mwisho kutumia huduma husika na baada ya hapo upulizaji dawa ufanywe kuua virusi wanaoweza kuwa wamebaki humo.
Kwa wanaotumia jiko pamoja na wengine PHE imeelekeza mgonjwa asitumie wakati wengine wakiwapo na ikiwezekana barakoa zivaliwe na vyakula viliwe kwenye vyumba vya wahusika wakiwa peke peke.
Ni zoezi ambalo si la mchezo mchezo – masharti ni mengi na kwa hakika lazima ushirikiano utolewe kwa kiasi kikubwa kutoka kwa waajiri ambao baadhi wameendelea kulipa mishahara kama kawaida na wengine wakiikata sambamba na posho. Lakini familia na rafiki wanaoishi pamoja lazima wawe katika ushirikiano wa hali ya juu ili kulindana.
Serikali iliweka bayana mapema orodha ya wafanyakazi muhimu ambao watoto wao lazima waendelee kupewa huduma za hali ya juu dhidi ya janga hili kuwaepusha. Hawa ni pamoja na wafanyakazi wa kada ya afya na huduma za jamii, wanaoendesha mfumo wa haki kama mahakama, polisi na magereza; wale wa kada ya dini, wa kwenye wakfu za kusaidia watu, waandishi wa habari na walio kwenye sekta ya usafirishaji.
Wengine ni wale walio katika sekta za uzalishaji, uuzaji na usambazaji wa huduma muhimu za kila siku pamoja na watawala.
Tumblr media
0 notes
magaratimes · 6 years
Photo
Tumblr media
#TRT: Wabunge nchini Marekani wasema kuwa mauaji ya Rohingya ni uhalifu wa kivita Wabunge nchini Marekani katika mkutano wao na Jeff Merkley wasema kuwa madhila yanayowakumbwa waislamu kutoka jamii ya Rohingya nchini Myanmar ni uhalifu wa kivita.
0 notes